AG FELESHI AKUTANA NA BALOZI WA SINGAPORE

Na Mwandishi Wetu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk. Eliezer Feleshi jana jumatatu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Singapore nchini Tanzania Mh. Douglas FOO.
Balozi Douglas FOO mwenye makazi yake Nchini Singapore alifika Ofisini kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.
Pamoja na kujitambulisha viongozi hao wawili walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Hii ni mara ya kwanza kwa Balozi Douglas FOO kukutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Balozi huyo wa Singapore yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo amekuwa akikutana na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Nchi ya Singapore inamahusiano ya kidiplomasia na nchi 150 duniani Tanzania ikiwamo.
30 Agosti 2022