AG FELESHI AWASHUKURU SAMIA NA JPM

Na Mwandishi Maalum
14/7/2022
Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, ameishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kuijumuisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Wizara ambazo zimepewa fedha za kujenga Majengo ya Kudumu katika Mji wa Serikali wa Mtumba, Jijini Dodoma.
Ametoa shukrani hizo leo, alhamisi, wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mji huo wa wa Serikali.
“Ninawashukuru sana Maraisi kwa maono yao na utambuzi wao wa kuiunganisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara mbalimbali katika awamu ya kwanza na ya pili ya ujenzi wa majengo ya kudumu hapa Mtumba. Hii ni heshima kubwa kwetu na hasa kwa kuzingatia unyeti wa majukumu yetu”. Akaeleza Mhe. AG
Katika ziara yake hiyo fupi na ambayo alikuwa ameambatana na Menejimenti yake, AG Feleshi amesema uamuzi wa Serikali wa kuwa na majengo ya kudumu ya serikali katika Mji wa Serikali wa Mtumba ni uamuzi wa kihistoria kwa vizazi na vizazi na umeufanya mji huo wa Serikali kuwa kivutio cha kitalii.
“ Majengo haya ni ya kudumu, ni historia kwa vizazi na vizani na kwa miaka mingi ijayo. Kwa hiyo nyinyi wakandarasi ambao mmepata fursa ya kujenga majengo haya lazima mjivunie historia hii kwa kufanya kazi wa uadilifu na kwa wakati, kwa sababu mnaandika historia”. amesisitiza AG Feleshi
Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lenye ghorofa tano na umbo la herufi Y linajengwa na Mkandarasi SUMA JKT Kanda ya Kati kwa gharama ya . Licha ya kuwa na umbo la herufi Y, litakapokamilika litakuwa ni kati ya majengo makubwa matatu katika majengo yote ya serikali yanayojengwa katika mji huo wa serikali pia ni moja ya majengo makubwa matatu katika majengo yote ya serikali yanayoendelea kujengwa katika mji huo wa Serikali.
AG Feleshi pamoja na kuridhishwa na namna kazi ya jenzi wa mradi huo unaotarajiwa kugharimu ....... mpaka kukamilika kwake amemtaka Mkandarasi kutosita kumpatia taarifa endapo kutakuwa na uchelewesashi wowote au urasimu kutoka pande zote mbili ( mteja na mkandarasi) ili aweze kuchukua hatua zozote.
“Mmenieleza hapa kwamba kwa sasa hamna changamoto kubwa, ila niwaombe kama kutakuwa na changamoto yoyote iwe kutoka Ofisini kwangu au kutoka Jeshini msisite kunijulisha ili hatua za mapema zichukuliwe. Lakini sisi ni wasimamizi wa Sheria, pia nisingependa kuona kunajitokeza matatizo yoyote ya kisheria kwenye mradi huu”.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia alijiridhisha kwamba fedha za utekelezaji wa mradi huo zimekuwa zikitolewa kwa wakati kila Mkandarasi anapowasilisha hati zake ( Certificate) na kwamba hakuna malimbilizo yoyote.
Awali akitoka maelezo ya maendeleo ya mradi huo Mshauri Mwelekezi Mhandisi William Sele kutoka Wakala wa Majengo ( TBA) alimweleza Mhe. AG na Ujumbe wake kwamba kazi ya ujenzi wa jengo hilo unakwenda vizuri kwa asilimia 26 ya ujenzi na kwamba hawategemei kupata changamoto kubwa labda uhaba wa mali ghafi hapo baadaye.
Mhandisi Sele pia amesema sasa hivi TBA inajitahidi sana katika usimamizi wa kazi zake ili kwenda na wakati na kuondoa malalamiko ya kwamba TBA wamekuwa wakishelewesha utekelezaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali.
“Sasa hivi kwa kweli tumejipanga vizuri, kazi zinakwenda kwa wakati, vibali vinatolewa kwa wakati, huko nyuma TBA tulikuwa tunalalamikiwa kwa ucheleweshaji wa vibali na mengineyo kama hayo, sasa tupo vizuri”, akasema Mhandisi Sele.
mwisho