Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
Bw. Akshai Fofaria Mwezeshaji kutoka Kampuni ya Sheria ya PINSENT MASONS LLP kutoka London Uingereza akimsikiliza mmoja wa maafisa
service image

MAFUNZO YAMETUONGEZEA MAARIFA- WAHITIMU

Na Mwandishi Wetu

16 Septemba 2022

Mafunzo  ya  siku nne ya kuwajengea uwezo maafisa wa serikali   katika maeneo ya  madini, gesi na mafuta yamehitimishwa leo kwa washiriki wa mafunzo hayo kukabidhiwa vyeti.

Jumla ya maafisa 37 wakiwamo  wa kutoka Ofisi ya Rais,  wameshirikia mafunzo hayo  ambayo baadhi yalitolewa kwa njia ya mtandao na mengine yalitolewa na wawezaji Bw. Akshai Fofaria kutoka Kampuni ya Sheria ya PINSENT MASON LLP   kutoka London Uingereza na  Bw  Aggrey Ernest Kutoka  Kampuni ya Sheria ya A&VC Tanzania.

Akihitimisha mafunzo hayo  Bi Aida Sylla mmoja wa waratibu wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya African Legal  Support Facility ameishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  kwa kuratibu mafunzo hayo na kuahidi tena kwamba  Taasisi ya  ALSF itaendelea kushirikiana na  Serikali ya Tanzania kupitia  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mafunzo hayo kuhusu  masuala  ya madini, mafuta na gesi ni awamu ya kwanza kati ya awamu tatu ambazo ALSF imeingia makubaliano na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo  wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema mafunzo yalikuwa ni mazuri na kwamba  katika siku nne  hizo za mafunzo  wamejengewa uwezo  lakini  wao wenyewe wamejengeana uwezo kutokana na  kwamba mafunzo hayo yalikuwa shirikishi.

“Kwangu mimi kama mchumi mafunzo yameniongezea  uwezo  na ufahamu wa mambo mengin yanayohusiana na  eneo hili ambalo  nisema ni nyeti na muhimu kwa  maendeleo ya nchi  yetu”. Akasema  Bw. Buji Bampebuye ambaye  ni   Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Naye Bi Upendo Ndosi ambaye pia ni mchumi  amesema licha ya kwamba mafunzo  hayo yameongeza uelewa katika eneo hilo lakini   aina ya ufundishaji,  fursa za kuuliza maswali, majadiliano katika makundi  ni mambo ambayo amesema yamewasaidia sana.

“Watu  tulikuwa huru kuuliza maswali na majadiliano  katika makundi pia yamesaidia sana katika kuongeza uwezo wa kuelewa. Lakini pia kupitia mafunzo  hayo tumejenga networking ambalo ni jambo  nzuri pia”. Akabainisha.

16 Sep, 2022
Maoni