Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
JOPO LA ITHIBATI YA WAENDESHA MARIDHIANO, UPATANISH, USULUHUSHI NA MAJADILIANO LAFANYA KIKAO CHAKE
service image

Na Mwandishi  wetu

 Jopo la Ithibati  ya waendesha  maridhiano, majadiliano,  upatanishi na usuluhishi  limekutana  chini ya Uenyekiti wa  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi.

Jopo  hilo   limekutana siku ya Jumatano ( January 11,2023) katika ukumbi wa Mikutano  uliopo  katika Kituo  Jumuishi ,Mahakama  Kuu  Kanda  Morogoro  ambapo   lilipitia, kujadili   kupitisha ama  kutopitisha  maombi kutoka kwa waombaji  kadhaa walioomba  kutoa huduma za maridhiano,  majadiliano,  upatanishi na usuluhishi.

 Jopo   linaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  ambaye ni Mwenyekiti  wajumbe wakiwa  ni  Wakili Mkuu wa Serikali  Dkt. Boniface Luhende, Rais wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea  Prof. Edward Hosseah,  Bi. Anita Malawo kutoka  Baraza la Taifa la Ujenzi na Bi. Madeline Kimei Rais wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania. Katibu wa  Jopo hilo ni  Wakili wa Serikali Mkuu   Abdulrahman Mshamu Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

 Jopo  la Ithibati ya waendesha maridhiano, majadiliano, upatanishi na usuluhishi     hukutana mara nne kwa mwaka  kupitia maombi ya waombaji  zikiwamo Taasisi zinazojihusisha na  utatuzi wa migogoro kwa njia  mbadala

 Waombaji wanaopitishwa baada ya kukidhi  vigezo  majina yao  hupelekwa kwa Msajili wa Watoa Huduma, Wizara ya Katiba na Sheria ambako  hupatiwa  usajili  

Takribani  waombaji  494 zikiwako Taasisi wamesajiliwa kuwa  waendeshaji wa  maridhiano, majadiliano, upatanishi na usuluhishi.

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano

January 14, 2023

14 Jan, 2023
Maoni