KUTOKA VIWANJA VYA NYERERE ( NYERERE SQUARE)DODOMA

Na Mwandishi wetu
23/01/2022
Maonesho ya Utoaji wa Huduma za Kisheria na Msaada wa kisheria yameingia katika siku yake ya pili ambapo Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali limepokea wananchi wa kada mbalimbali waliofika kupata huduma za ushauri na msaada wa kisheria.
Maonesho haya yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa mwaka mpya wa Mahakama mwaka ambao utazinduliwa rasmi February Mosi 2023 katika Viwanja vya Chinangali.
Leo (jumatatu) Jaji kiongozi Mhe. Mustapher Siyani leo alitembelea baadhi ya mabanda na kupewa taarifa mbalimbali kutoka kwa wahudumu wa mabanda hayo naye alitoka maagizo kadhaa.
Wateja ambao wanatembelea Banda la OMMS kupata huduma wamekuwa wakiomba kupewa ushauri na masaada wa kisheria katika maeneo mbalimbali yakiwamo maswala ya ajira, hukumu zilizotolewa na mahakama, na wengine wakiitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia uwezekano wa Kwenda maeneo ya nje ya Jiji la Dodoma ili kutoa elimu ya sheria na msaada wa kisheria kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini.
Ujumbe wa mwaka huu ni Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi katika Kukuza Uchumi Endelevu Wajibu wa Mahakama na Wadau.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mdau wa mahakama katika kuutekeleza kwa vitendo ujumbe huo, Mwaka 2020 OMMS ilitoa mwongozo maalumu ambao ulizishauri na kuzitaka Taasisi za Serikali zinapoingia kwenye migogoro zitumie njia za usuluhishi kwanza, chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya kukimbilia mahakamani .
Mawakili wa Serikali wanohudumu katika Banda hili ni Angela Kimaro, Hery Sanga na Sindeyan Suyaani.
Imeandaliwa Kitengo cha Mawasiliano