Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
MKANDARASI JENGO LA MWANZA ASHAURI KUANZA MCHAKATO WA LIFT
service image

Na  Mwandishi wetu

20 Septemba 2022

 

Mkandarasi  (SUMA JKT)anayejenga jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika eneo la Buswero  Mkoani Mwanza , ameushauri  uongozi wa OMMS kuanza  mapema mchakato wa ununuzi wa lifti kwaajili ya matumizi jengo hilo.

Ushauri huo umetolewa  jana ( jumatatu) na  Luteni Kanali Mhandisi Fabian Buberwa kutoka SUMA JKT   wakati alipokuwa akitoa maelezo  kwa Mkurugenzi wa Mipango wa  OMMS  Bw Buji Bampabuye  kuhusu  maendeleo ya  Ujenzi wa mradi

Mkurugenzi  Bampabuye   anakagua maendeleo ya  mradi huo  kwa maelekezo ya Naibu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa ili kupata  taarifa za kina na za uhakika za maendeleo ya mradi huo.

Kwa mujibu wa M Mkandarasi Buberwa ambaye  pia ni  Meneja wa Kanda wa Suma JKT kwamba  kwa uzoefu wake mchakato wa  kununua lift hushukua  kati ya miezi miwili hadi  mitatu baada ya jengo  kukamilika hivyo ni vema mchakato huo ukaanza mapema.

Kuhusu  maendeleo ya mradi huo  ambao  hadi kukamililka kwake utagharimi Shilingi Bilioni 3. Lt Col Buberwa amesema   kwa ujumla ujenzi wa jengo hilo lenye gorofa   tatu unakwenza vizuri na matarajio ni  likamilike  kwa wakati au kabla ya wakati kulingana  na mkataba.

“Matarajio yetu ni jengo   litakamilike mapema sana mpaka ifikapo  Mwezi Desemba  mwaka huu  ujenzi   labda  unaweza  kukamilika na  umaliziaji ( finishing) kati ya februari au Machi, lengo letu ni kukabidhi jengo mwezi March 2023. Nitoe ushauri kwamba mchakato wa manunuzi ya lift uanze mapema kwasababu mchakato wake kwa uzoefu wangu  huweza kuchukua kati ya mienzi mitatu  hadi mine”. Amesema  Lt Col Buberwa.

Akielezea  zaidi   umuhimu kuanza mchakato huo mapema,  Msimamizi wa Mradi huo Lt. Col Buberwa  amesema jengo hilo  halina njia ya watu wenye ulemavu kwa hiyo tegemeo  kubwa  na  uwepo wa Lift.

 Mkandarasi huyo amesema hadi sasa  gorofa ya chini ( ground floor) imeshakamilika  kwa kujenga matofali floor yote na vyumba vyote katika floor hiyo vimekamilika.

“Zege katika floor ya kwanza limeshamwaga na  tarehe   20 septemba 2022   tutataanza kufanya  setting  ya gorofa ya pili ikiwamo kazi ya  kusuka nondo na slabu ya gorofa ya pili, lakini  niseme kwamba kazi ya ujenzi  wa kuta za floor ya kwanza inakwenda sambamba na  setting ya floor ya pili”. Akabinisha.

Amesema  ujenzi wa  mradi huo unakwenda kwa kasi kutokana na  ushirikiano  mkubwa anaoupata  kutoka kwa mwenye  mradi( OMMS) na hasa suala  la ufuatiliaji wa mara kwa mara

“Nawashukuru sana OMMS kwa kuja  mara kwa mara kututembelea. Nimefanya kazi hii kwa miaka 15 lakini  sijaona ushirikiano kama huu wa OMMS ni mradi wa kwanza  ninaoufurahia kuusimamia na  ndiyo mrdsi ambao naamini utakamilika mapema zaidi. Ninayo miradi  hapa ina miaka mine  haijakamilika, nyinyi mmeanza juzi tu  lakini mradi unakwenda vizuri”. Amebainisha  Lt. Col Buberwa

Amefafanua zaidi kwa kusema   ushirikiano huu  naupata  pia kutoka kwa Mkuu wa Taasisi. “Namshukuru sana  Mhe. Mwanasharia Mkuu  wa Serikali  amewahi  pia kunipigia simu na kuuliza kama kuna changamoto yoyote katika mradi, hili  halijawahi kutokea kwa kiongozi yoyote. Hii  inatupa ari ya kuendelea kuchapa kazi na tunalipwa kwa wakati”

Kwa upande wake Mhandisi Mkazi wa Mkoa wa mwanza. Bw. Mosses Urio  kutoka TBA yeye amesema kwa sasa  hakuna changamoto yoyote na jengo anatarajia likamilike kwa wakati  licha ya  kuwa nyuma kwa siku 4   ambazo wameelekeza mkandarasi kuzifidia katika hatua ya ujenzi wa floor ya pili.

Akaongeza kwa kusema,  wanahakikisha  specimen zote zinapimwa chini ya usimamizi wao, kuwa na vikao vya mara kwa mara na kwa wakati na kwamba  Mkandarasi  anaendelea vizuri na hakuna deni lolote analodai.

Akizungumza kwa  niaba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Mkurugenzi Bampebuye amepongeza kwa hatua nzuri ya ujenzi  ya mradi huo na kuwahakikisha ushirikiano ili  mradi ukamilike kwa wakati kama alivyoahidi.

Jengo la  OMMS linalojengwa Mkoani Mwanza  kwa usimamizi wa  OMMS  ni Jengo la Kwanza   Jumuishi  litakalotumiwa   pamoja na Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

 

 

 

20 Sep, 2022
Maoni