MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA ATEMBELEA BANDA LA OMMS

Na Mwandishi wetu
Nyerere Square
24/1/2023
Katika siku ya Tatu ya maonesho ya Wiki la Sheria, Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali limetembelewa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma
Wakili wa Serikali Angela Kimarao ndiye aliyetoa maelezo kuhusu majukumu ya jumla ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu lakini pia akabainisha jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zikiwamo za kusimamia usuluhishi wa migogoro baina ya taasisi za serikali.
Wakili wa Serikali Angela Kimaro pia alimueleza Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kwamba, katika eneo la utoaji huduma za msaada wa kisheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia inayo namba ya bure ambayo wananchi wanaweza kupiga simu na kuomba ushauri au msaada wa kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Pia alielezea majukumu mbalimbali ambayo OMMS inaendelea kutekeleza kuwa ni pamoja na kutafsri sheria kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili pamoja , Urekebu wa Sheria mbalimbali na upembuki wa mikataba.
Kwa Upande wake Mhe Wilibert Chuma alitaka kupata ufafanuzi wa namna gani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inachukua jukumu la kuwaelimisha wananchi utofauti kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali .
Vilevile Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania alitaka kufahamu kama kumekuwa na upungufu wa mashauri yanayoihusu serikali kufuatia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka Mwongozo wa mwaka 2020 ambao ulitoa maelekezo kwa Taasisi za serikali kuchukua njia mbadala za usuluhishi badala ya kukimbilia mahakanami.
Msajili wa Mahakama aliridhishwa na ufafanuzi aliopewa na akaipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake. ikielimisha umma kuhusuAkiwa katika Banda la OMMS alielezwa kwa muhtasari kuhusu majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika ujumla wake.
Pamoja na ugeni wa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Banda la OMMS limepokea wananchi wa kada mbalimbali waliofika kuomba ushauri na msaada wa kisheria au walitaka kuelimishwa majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Vile vile Mhasibu wa Muda wa Chama cha Mawakili wa Serikali Irene Lesulie ameshirikia na Mawakili wa Serikali kutoka OMMS katika kuwahudumia wananchi
Imeandaliwa na Kitengocha Mawasiliano