OFISI YA MWASHASHERIA MKUU WA SERIKALI YAPATIWA VIFAA VYA TEHEMA

OFISI YA MWASHASHERIA MKUU WA SERIKALI YAPATIWA VIFAA VYA TEHEMA
Na Mwandishi Maalum
Makampuni ya Supperdoll na Kagera Sugar yametoa vifaa vya kisasa vya TEHAMA ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali na hususani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali za kuimarisha na kuboresha utekelezaji wa majukumu yake kupitia mawasiliano ya kisasa ya TEHAMA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni hayo Bw. Seif Ally Seif akiongozana viongozi wengine kutoka makampuni hayo jana ( Jumatatu) alimkabidhi Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi, Komputa za kisasa za mezani 5 ( Desktop), Komputa mpakato za kisasa 5 ( laptop) na Printa ya kisasa moja katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma.
Kupatikana kwa vifaa hivyo kuna tokana na mazungumzo ya awali yaliyowahi kufanyika kati ya AG Feleshi na uongozi wa Makampuni hayo ambapo AG pamoja na mambo mengine alielezea mweleko wa Ofisi yake na hamu kubwa ya kuona Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inakuwa na vifaa vya kisasa vya Tehama na ndipo Uongozi wa Makapuni hayo ulipoahidi kusaidia.
Akikabidhi vifaa hivyo, Bwa. Seif Ally Seif alimweleza AG Feleshi kwamba, Makampuni yake yataendelea kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Serikali kwa ujumla kwa kadri ya uwezo wake.
Akipokea vifaa hivyo, AG Feleshi akiwa na viongozi wengine kutoka Ofisi yake, pamoja na kushukuru kwa msaada huo. Amesema, Ofisi itahakikisha inavitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuwahudumia wadau wake ndani ya serikali na nje ya serikali kwa weledi na kwa wakati.
Aidha AG Feleshi ameahidi kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wake wote.
28/6/2022