PONGEZI TUNAZOPEWA ZIWE CHACHU KWETU-AG FELESHI

Na Mwandishi wetu
14 June 2022
Kufuatia pongezi nyingi ambazo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekuwa ikizipata, huku nyingine zikitolewa mubashara. Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amewaasa watumishi wa Ofisi hiyo kuzitumia kama chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi, bidii, uadilifu, ubunifu na kwa wakati.
Ameyasema hayo katika salamu zake za pongezi kwa watumishi wa OMMS alizozitoa kupitia Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa ambapo amemtaka kuzifikisha pongezi hizo kwa Watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika salamu zake hizo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili Ofisi katika utekelezaji wa majumuku yake, amekuwa akipokea salamu nyingi za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali wanaopata huduma zao kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
“Pamoja na changamoto zinazoikabli Ofisi yetu ambazo tumeendelea kuzifanyia kazi kwa lengo la kuboresha zaidi huduma zetu kwa wadau wetu, hivi karibuni Divisheni ya Mikataba imeongeza sana kasi ya kushughulikia kazi zake kwa weledi na kwa wakati pamoja na ukweli kwamba, mikataba mingine imekuwa ikiwasilishwa Ofisini kwetu kwa kuchelewa na ikiwa na mapungufu mengi” amesema AG
Amebainisha kwamba, mapema mwezi huu wa June, alihudhuria hafla ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikuwa anashuhudia utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.
“ Katika hafla hiyo, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilipongezwa kwa dhati kwa jinsi ilivyotekeleza majukumu yake katika upekuzi wa mikataba husika kwa weledi na kwa wakati licha ya baadhi ya mikataba hiyo kuwasilishwa kwa kuchelewa sana na ilitakiwa kutiwa saini ili kuruhusu hatua za utekelezaji kuanza” amesema AG.
Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Maji Injinia Anthony Sanga alisema.
“ Lakini Mhe. Rais, naomba sana sana nisiache kumshukuru Mhe. Jaji Dk. Feleshi kwa kazi kubwa na nzuri sana ambayo ametusaidia Mwanasheria wetu Mkuu wa Serikali, mikataba mingine ilikwenda asubuhi na ikatoka jioni,kwa maana imefanyiwa upekuzi ndani ya siku moja , tunamshukuru sana Jaji Feleshi”.
AG Feleshi amekwenda mbali kwa kubainisha pia kwamba, pamoja na pongezi hizo zilizotolewa mubashara tarehe 6/6./2022 , amekuwa akipokea mrejesho na pongezi za namna hiyo kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusiana na huduma za kisheria zinazotolewa na Divisheni ya Uandishi wa Sheria na Ile ya Uratibu na Ushauri wa Sheria.
“ Kwa namna ya pekee, nimeona inafaa na ni jambo muhimu nikuletee ( DAG) ili ufikishe pongezi hizi kwa Mkurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi wa Divisheni ya Mikataba pamoja na Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na watendaji wote wa Divisheni zingine na kuwaomba waendelee kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na kushughulikia kazi zinazotolewa kwetu kwa wakati” amesisitiza Mhe. Feleshi.
Akaongeza kwa kusema. “ Naomba pongezi hizi ziwe chachu kwa watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi, bidii, uadilifu, ubunifu na kwa wakati kwa maslahi ya umma kwani naamini kazi zetu zinatekelezwa kwa kupokezana mfano wa mnyororo ambapo kila afisa anayehusika kwa ngazi yake anachangia kutoa matokeo chanya ya kazi zetu”.
Wakati huo huo, AG Feleshi amesema , anapowasilisha pongezi hizi, anawaomba watumishi wote kuongeza kasi ya kukamilisha mpango wetu wa kutumia TEHAMA katika kupokea, kuchakata na kuwasilisha matokeo ya kazi zetu kwa wadau.
Mwisho.