UONGOZI MPYA WA TLS WAJITAMBULISHA KWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

• Waomba udhibiti Mawakili Vishoka
• Awataka kuepukana na Uanaharakati
Na Mwandishi Maalum
Uongozi mpya wa Chama cha Mawakili Cha Tanganyika (TLS) umejitambulisha rasmi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi.
Viongozi hao ambao ni Baraza la Uongozi (Governing Council) wakiongozwa na Rais wa TLS Bw. Harold Sungusia waliomba kumtembelea (courtecy call) na kufanya mazungumzo Mwanasheria Mkuu wa Serikali mnamo tarehe 10 Agosti, 2023 katika Ofisi yake mkoani Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, pamoja na kujitambulisha kwa Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, viongozi hao wa TLS waliwasilisha na kujadiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali masuala mbalimbali yanayohusu Chama hicho (TLS) na Tasnia ya Sheria katika ujumla wake.
“Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali tuliomba kuja kukutana nawe kama sehemu ya kujitabulisha au kuutambulisha Uongozi mpya wa TLS lakini kubwa zaidi ni kujenga uhusiano mzuri na ushirikiano baina ya Serikali na TLS”, alisema Rais wa TLS Bw. Harold Sungusia.
Masuala ambayo uongozi wa TLS uliwasilisha na kumwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali awasaidie ni pamoja na mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Chama cha Mawakili Tanganyika ambayo yalitarajiwa kuwasilishwa kwenye Kikao cha Bunge la mwezi Januari, 2023.
Bw. Sungusia alisema, "TLS iliwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya TLS na ilitarajia mabadiliko hayo yangewasilishwa kwenye Kikao cha Bunge cha Mwezi Januari, 2023. Kwa kuwa bado mabadiliko ya Sheria hiyo hajawasilishwa Bungeni, tunakuomba Mwanasheria Mkuu utusaidie kuwasilisha mapendekezo hayo Bungeni.”
Aidha, hoja nyingine iliyowasilishwa na Uongozi wa TLS kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Feleshi ilihusu kutambua mihuri ya kielectroniki.
Katika hoja hii, TLS ilieleza na kubainisha kwamba, mihuri ya kielektroniki iliwekwa kwa ajili ya kuepusha vishoka. Hata hivyo, kwa mujibu wa TLS, Sheria ya Makamishna wa Viapo (The notaries and Public and Commissioners for Oaths) imetambua Mawakili wa Serikali na Mahakimu kama Makamishna wa viapo.
Vile vile, vifungu namba 10 na 11 vimetoa nguvu kwa baadhi ya Maafisa ambao sio Mawakili kuweza kutoa viapo. "Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, suala hili linasababisha ongezeko la vishoka. Hivyo, TLS inapendekeza kuwe na marekebisho ya Sheria hii na kuacha nguvu ya kutoa viapo kwa Mawakili. Pia, tunapendekeza kuwe na kikosi kazi cha kuchunguza matumizi ya mihuri iliyo sahihi kwa Mawakili”. Aliongeza Rais wa TLS.
Ushirikishwaji wa mawakili binafsi kwenye kesi za umma ni pendekezo jingine lililowasilishwa na Uongozi wa TLS kwa Mwanasheria Mkuu ambapo katika eneo hili, TLS iliomba kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Serikali iwe inawatumia pia Mawakili binafsi katika uendeshaji wa mashauri ya umma na kwenye miradi mikubwa ya Serikali.
Vile vile, TLS imeomba Mawakili Vijana kupewa fursa ya kujifunza ili kukuza na kuwajengea uwezo kwenye maeneno mbalimbali ya Kisheria.
Katika kikao hicho, TLS waliomba pia kuangalia au kupitia Taratibu za kukazia hukumu dhidi ya Serikali. TLS walimfahamisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba, Taratibu za kukazia Hukumu dhidi ya Serikali ni ngumu na kusababisha wadau kuchelewa kupata haki na hivyo kuomba taratibu hizo ziangaliwe upya.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, akijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwake na Uongozi wa TLS, pamoja na kuupongeza Uongozi mpya na TLS kwa ujumla kwa kazi nzuri, amekitaka Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS) kiwasilishe Sheria zote zinazohitaji marekebisho Wizara ya Katiba na Sheria.
Aidha, Mhe. Jaji Dkt. Feleshi aliuambia Uongozi huo kwamba, Mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya TLS yatawasilishwa Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria kwenye Kikao cha kumi na mbili (12) cha Bunge.
Kuhusu hoja ya Mawakili wa Kujitegemea kuendesha mashauri mbalimbali ya Umma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Serikali imekuwa na itaendelea kufanya kazi na Mawakili wa Serikali katika uendeshaji wa mashauri hayo na kwamba, Serikali inawakaribisha Mawakili binafsi kufanya kazi na Serikali.
Hata hivyo, pamoja na utayari wa Serikali wa kufanya kazi na Mawakili binafsi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameitaka TLS kuainisha na kuwasilisha Serikalini ujuzi wa Mawakili wake pamoja na maeneo ya ubobevu ili Serikali iweze kuwatumia pale kunapokuwa na uhitaji.
Kuhusu suala la kuwaondoa maafisa ambao si wanasheria kuchukua viapo, Mwanasheria Mkuu ameitaka TLS kuwasilisha mapendezo ya kuondoa nguvu hizo kwa maafisa ambao si wanasheria kuchukua viapo ili yafanyiwe kazi.
Kwa upande wa kuwaendeleza na kuwajengea uwezo na maarifa Mawakili Vijana, Mwanasheria Mkuu amewataka Mawakili Waadamizi kufungua milango ya kuwafundisha Mawakili Vijana(mentorship) na akaitaka TLS kuwa wabunifu zaidi ya namna bora ya kuwasaidia Mawakili Vijana.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,ameshauri kuangaliwa upya mfumo wa Sheria nchini na ikiwezekana kufungua milango ya watu wa kada mbalimbali kusoma Sheria kama shahada ya pili ili kuongeza uwezo wa Mawakili.
Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amewahimiza na kuwaasa Mawakili wote kuongeza uadilifu na uwajibikaji hasa kwa kuzingatia kwamba wao ni Mawakili na Maafisa wa Haki na hivyo kipaumbele chao kiwe ni utoaji na usimamiaji haki na si fedha.
Mhe. Jaji Dkt. Feleshi kupitia TLS ametoa wito kwa Mawakili wote kuzingatia umuhimu wa ushirikiano na kusaidiana kwa maslahi ya Watanzania na Taifa kwa ujumla wakati huo huo akawekea mkazo haja ya kupunguza uanaharakati hasa kwa masuala yanayohusu utaalamu ili kutoa fursa kwa wanataaluma kuyashughulikia kitaalamu na kwa dhamiri yenye Uzalendo na maslahi kwa Taifa.
Mwisho.
13/8/2023

“Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali tuliomba kuja kukutana nawe kama sehemu ya kujitabulisha au kuutambulisha Uongozi mpya wa TLS lakini kubwa zaidi ni kujenga uhusiano mzuri na ushirikiano baina ya Serikali na TLS”, alisema Rais wa TLS Bw. Har