VIONGOZI WA TUGHE TAWI LA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WAASWA KUWA WAADILIFU

Na Mwandishi Maalum
Dodoma
15/11/2022
Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Tawi la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameaswa kuwa waamini na waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Rai hiyo imetolewa leo ( Jumanne ) na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya wanachama wa TUGHE tawi la ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mafunzo hayo yametolewa na viongozi wa Tughe Mkoa wa Dodoma na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mtumba, Jijini Dodoma.
“Nitoe rai kwenu viongozi wa TUGHE muonyeshe uadilifu na uaminifu ili wanachama wenu wawe na imani kwenu lakini pia wajue michango yao inatumikaje tumikaje , je inatumika vizuri na kwa manufaa yao?” akasema na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Akaeleza pia kuwa, kwa viongozi kuonyesha uadilifu na uaminifu kutawafanya wanachama waliopo waendelee kukipenda chama chao, lakini uandilifu huo na uaminifu utawavutia wanachama wapya.
Akizungumzia kuhusu mafunzo nayo, Dkt. Longopa ameelezea kufurahishwa kwake na mafunzo hayo ambayo ameyataja kuwa ni muhimu kwa wanachama kwani yatawawezesha kuwa na uelewa wa Pamoja kuhusu chama chao.
Akasema Chama cha Wafanyakazi sehemu ya kazi ni chambo muhimu sana hasa katika kutetea haki, maslahi na maendeleo ya wafanyakazi.
Ni kwa sababu hiyo, amewataka viongozi hao wa TUGHE tawi la OMMS kuhakikisha wanaongeza jitihada za kuwahamasisha wanachama wapya hasa wale ambao hawana vikwanzo vya kisheria kujiunga.
“ Wafanya kazi wengi bado hawafahamu manufaa na faida za kujiunga na TUGHE, mwanachama anapopata shida mahali pakazi na pale menejimenti inapotaka kumpatia adhabu, TUGHE mahali pa kazi huwa wanakuwa na mchango mkubwa wa kumterea mfanyakazi yule na mara nyingi TUGHE imekuwa ikiwasaidia sana wanachama sehemu ya kazi” akasisisita DAG .
Akaongeza kuwa inakuwa rahisi sana kwake kukutana na uongozi wa TUGHE kwa niaba ya wafanyakazi badala ya kukutana na mfanyakazi mmoja moja, kwa hiyo wafanyakazi watambue umuhimu na nafasi ya TUGHE katika kutetea maslahi na haki zao kwa kujiunga na TUGHE.
Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo hayo ambaye ni Katibu TUGHE Mkoa ( Dodoma) Bw. Samuel Nyungwa pamoja na kuelezea chimbuko la TUGHE pia alisisitiza haja na umuhimu kwa viongozi kuwa na uwazi hasa katika masuala ya fedha kwa kutoa taarifa sahihi.
Bw. Samuel Nyungwa pia katika mafunzo amefafanua haja na umuhimu wa TUGHE tawi la OMMS kuwa daraja la mawasiliano na maridhiano baina ya wafanyakazi na Menejimenti.
Akabainisha kwamba inapokuja suala la kutetea maslahi , haki na maendeleo ya wafanyakazi, Viongozi wa TUGHE wanawajibika kuwakilisha makundi yote bila ya kubagua.
Bw. Nyungwa amezitaja nguzo tatu muhimu za TUGHE ambazo ni umoja wa wanachama, uhuru na demokrasia.
Mada ambazo nzime tolewa katika Mafunzo hayo ni Pamoja umuhimu wa chama cha wafanyakazi mahali pa kazi, na namna bora ya uendeshaji wa chama ili wanachama washiriki kikamilifu katika chama chao mada iliyotolewa na Afisa Elimu TUGHE Nsubisi Mwasandende na namna bora ya kuwa na mahusiano mazuri na menejimenti
Awali akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo , Katibu wa TUGHE tawi la OMMS Bi, Dorina Kalumuna amesema kwa sasa TUGHE Tawi la OMMS linawachama 54.
Pamoja wanachama wa TUGHE kushiriki mafunzo hayo, wengine walioalikuwa kushiriki walikuwa ni wajumbe wawakilishi kutoka Divisheni na Vitengo vya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali .